Timu ya Taifa ya Baseball leo imetembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kupokelewa na Mhe. Balozi Dr. Pindi Chana. Balozi amewaasa wachezaji kucheza kwa hali ya juu na hatimaye waliwakilishe vema Taifa letu katika Mashindano ya Africa Zone East Olympic games Qualifiers yatakayoanza Kesho jijini Nairobi katika viwanja vya shule ya Lenana.Timu mbili za juu zitafuzu kuelekea finals nchini Afika Kusini kuanzia tarehe 1-5 Mei, 2019.Mpaka sasa timu zilizothibitisha ni Kenya, Uganda na Tanzania.Zambia imeshindwa kushiriki.