Tarehe 30 Agosti 2019, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alichukua rasmi uenyekiti wa Mabalozi wa kutoka nchi za SADC na kuongoza Kikao cha Mabalozi hao. Kikao kilifanyika katika Hoteli ya Sankara iliyopo Nairobi. Baada ya Kikao, Mhe. Balozi Chana alizungumza na vyombo vya habari kuelezea maazimio ya Kikao hicho.