Balozi Dkt. Pindi Chana amemtembelea Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji wa Kenya Mhe. Mwangi Kiunjuri leo tarehe 16 Aprili 2018. Katika mazungumzo yao, viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Kilimo na Umwagiliaji. Aidha, Balozi Chana alitumia fursa hiyo kumualika Waziri Kiunjuri katika Maonesho ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya yatakayofanyika tarehe 25-28 Aprili 2018, Nairobi, Kenya.